Mix

Benki ya NMB wamesogeza zaidi huduma jirani yako kwa hii ya MaxMalipo

on

IMG_6662

Mkazi wa kigamboni akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa NMB.

Benki ya NMB imeanza kutoa huduma zake kupitia mawakala wa MaxMalipo kwa mafanikio katika hatua ya majaribio ambayo inaendelea maeneo ya Kigamboni Dar es Salaam, Dodoma na Arusha.

Huduma hiyo inayojulikana kama NMB Wakala itakuwa inapatikana kwenye maduka ya kawaida yenye huduma za MaxMalipo, inategemea kusogezwa mpaka vijijini na kuwa benki ya kwanza kupenya maeneo ya vijijini.

IMG_6790

NMB inafanya matangazo katika eneo la Kigamboni kuhamasisha wakazi wa eneo hilo wanapata elimu zaidi ya jinsi ya kutumia huduma ya NMB wakala ambapo mtu yeyote anaweza kufungua akaunti na kupata Kadi ya ATM papo hapo.

Majaribio yaliyofanywa eneo la Kigamboni Dar es Salaam limeonyesha mafanikio makubwa hivyo NMB inajipanga kuisogeza huduma hii nchi nzima huku malengo ya awali ikiwa ni kuwa na mawakala zaidi ya ya 3,000.

IMG_6768

Burudani ilisogezwa pia na NMB wakati wa kutoa elimu ya huduma hiyo.

IMG_6808

IMG_6813

IMG_6852

Unataka niwe nakusogezea kila kinachonifikia? Ungana na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram kwa kubonyeza hapa ili niwe nakutumia kila kitu moja kwa moja >>>Facebook Twitter Instagram

Tupia Comments