April 16 2016 ni siku ambayo wakazi wa kigamboni walianza kulitumia daraja la ‘Nyerere’ Kigamboni na baaadae Daraja la Nyerere ‘kigamboni’ lilifunguliwa rasmi April 19 2016 na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John pombe Magufuli.
Afisa Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) David Mziray ameongelea uanzishwaji wa usafirishaji wa abiria kwa daladala kupitia daraja la Nyerere ‘Kigamboni’ Dar es salaam…
>>>‘tunaomba kuamasisha wamiliki wa mabasi kuja kupata leseni kwa ajili ya kutoa huduma ya Kigamboni kwenda mbagala rangitatu, kigamboni kwenda temeke, kigamboni- stesheni, sasa hivi njia hizo ziko wazi, tunaamasisha magari ambayo yanabeba abiria 27 na kuendelea, nauli zinaanzia 400 mpaka 450‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ULIIKOSA HOTUBA YA RAIS MAGUFULI WAKATI WA UZINDUZI WA DARAJA KIGAMBONI? BONYEZA PLAY HAPA CHINI