Gumzo jingine mtandaoni ni video fupi inayosambaa ikimuonesha Kijana Raia wa Congo aitwae Muima akitangaza kwa ujasiri kwamba anafunga ndoa na Mpenzi wake aitwae Thereza ambaye ni Bibi wa miaka 85.
Mtandao wa Citizen Kenya umemnukuu Muima akiongea na Mwandishi wa habari na kusema maneno yafuatayo “Sitachagua yeyote badala yake ingawa yeye ni Mwanamke mzee na kwa kweli anaweza kuwa bibi yangu lakini bado ninampenda, hili ni chaguo langu, hii ni furaha yangu na kabla ya kuwafurahisha wengine kwanza jipende mwenyewe sio kwa kuzingatia maoni ya Mtu mwingine.”
Akisimulia mahusiano yao, Muima alisema kuwa mara ya kwanza yeye na marafiki zake walikuwa wameenda kuwinda karibu na nyumba inayomilikiwa na Thereza ambapo baada ya miezi michache kupita ndipo Thereza akaanza kumpenda.
Thereza ana watoto nane na Wajukuu 20 na anasema anatarajia kuolewa na mpenzi wake huyo wa siku nyingi “nina Watoto nane na Wajukuu 20, kulingana na umri wa Mpenzi wangu anaweza kuwa Mjukuu wangu wa tano, ananipenda na mimi nampenda, niko tayari kuvaa vazi la harusi na pete katika siku yetu ya harusi” via Citizen Kenya.
KOREA KASKAZINI YAMUUNGA MKONO PUTIN, TANZANIA YAENDELEA KUSIMAMA KATIKATI, KENYA WABADILI MSIMAMO