Wizara ya Afya inaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu hali ya ugonjwa wa UVIKO-19 nchini ambapo katika kipindi cha tarehe 05 Machi hadi 03 Aprili 2022, kuna jumla ya maambukizi mapya 116 ya waliothibitika kuwa na maambukizi kati ya Watu 25,890 waliopimwa ambayo ni sawa na asilimia 0.45.
“Tukumbuke kuwa ugonjwa huu kwa mara ya kwanza ulitolewa taarifa hapa nchini mnamo mwezi Machi 2020 na kufikia tarehe 03 Aprili 2022 watu 33,842 walikuwa wamethibitishwa kuwa na maambukizi kukiwa na jumla ya vifo 803, katika kipindi cha 05 Machi hadi 03 Aprili, 2022, Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuwa na idadi kubwa ya watu waliothibitika kuwa na maambukizi (watu 70) sawa na asilimia 60.3 ya maambukizi hayo”
“Katika kipindi cha tarehe 05 Machi hadi tarehe 03 Aprili 2022, jumla ya wagonjwa wapya 22 walilazwa, wagonjwa hawa wote walikuwa hawajachanjwa, aidha kwa siku ya tarehe 03 Aprili 2022, wagonjwa mahututi walikuwa wawili (02) na wote walikuwa hawajapata chanjo ya aina yoyote ya kukinga dhidi ya UVIKO – 19”
“Katika kipindi cha taarifa hii, jumla ya vifo vitatu (03) vimeripotiwa kutoka mikoa ya Dar es Salaam (2) na Mwanza (1), Idadi hii inaonyesha kupungua kutoka vifo nane (8) vya mwezi uliotangulia, vifo vyote vilivyoripotiwa vilikuwa vya wagonjwa ambao hawakupata chanjo ya aina yoyote ya kukinga dhidi ya UVIKO – 19”
KOREA KASKAZINI YAMUUNGA MKONO PUTIN, TANZANIA YAENDELEA KUSIMAMA KATIKATI, KENYA WABADILI MSIMAMO