Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima amekemea vikali tabia ya watumishi wa sekta ya Afya kudanganya na badala yake amewataka kuwa weledi katika utumishi wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Gwajima amesema hayo jana wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Mkoani Mwanza na kubaini kuwepo malalamiko ya uhaba wa dawa kutoka wananchi yaliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Cornel Magembe.
Aidha, Dkt. Gwajima ameshangazwa kusikia wagonjwa hawapewi Paracetamol lakini alivyotembelea stoo akakuta dawa hizo zipo.
Pia namna mnyonyoro wa dawa unavyoendeshwa katika Hospitali hiyo umemshangaza Dkt. Gwajima kwani inaonekana kuna uzembe na ubadhirifu mkubwa wa dawa na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali.
MAPYA YA ‘MGANGA’ WA SIMBA “ANGEFUNGA ANGEKUFA, NINA PAKA 40, BILA UCHAWI HAWASHINDI”