Unaweza usiamini lakini ukweli ndio huo mtu wangu, Unaambiwa kaka wa damu wa mwanadada Kim Kardashian hajahudhuria harusi ya dada yake kwa madai ya kuchoshwa na jinsi dada yake huyo pamoja na mumewe Kanye West wanavyofanya vurugu nyingi za maonyesho ya mali na nguo.
Siku hiyo ya harusi kaka huyo wa Kim, Rob Kardashian, alionekana katika Uwanja wa ndege wa Los Angeles alikosafiri na mama yake muda ambao Kim na Kanye walikuwa wakifunga ndoa mjini Florence Italia.
Taarifa nyingine zinadai kuwa Kim pia alikasirishwa na kitendo cha kaka yake huyo kushindwa kupunguza unene alionao kutokana na kwamba angetokea vibaya kwenye picha za familia.
Rob hakuacha kuhudhuria harusi hiyo peke yake bali pia aliacha kushiriki kila kitu kilichoandaliwa na familia yake ikiwa ni pamoja na ile Pre Wedding Party, Alipoulizwa kwanini hakushiriki harusi ya dada yake Rob hakujibu chochote. Mtoto huyo pekee wa kiume katika familia ya Kardashian hajaonekana hadharani tangu January mwaka 2014 baada ya kuamua kukaa mbali na macho ya watu kutokana na kuongezeka unene wa kupindukia.
Unapenda stori kama hizi zisikupite? niko tayari kukutumia wakati wowote mtu wangu, jiunge na mimi kwa kubonyeza >>> Twitter Instagram facebook na kupata pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.