Kutokana na mwanadada Kim Kardashiankusaidiakurekebisha mfumo wa sheria za magereza na hukumu kwa wafungwa basi umepelekea kuachiwa huru kwa mfungwa mmoja aitwaye Matthew Charles ambapo miezi kadhaa iliyopita Kim alimsaidia mwanamama Alice Johnson kutoka jela.
Matthew Charles alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 35 kwa kosa la dawa za kulevya na kumiliki silaha bila kibali chochote tokea mwaka 1996 ambapo inaelezwa kuwa tayari ameshatumikia miaka 20 mpaka sasa. Huku taarifa zilizosambaa ni kuwa mapema mwaka huu aliachiwa kwa msamaha wa Rais Donald Trump.
Kim Kardashian alionekana kutatua tatizo lililokuwa likimkabili Matthew baada ya kuachiwa huru huku ikielezwa kuwa Matthew alipata wakati mgumu wa kupata nyumba kutokana na makosa yaliyokuwa yakimkabili na kukataliwa sehemu mbalimbali, hivyo Kim aliamua kumlipia kodi ya miaka mitano.
VIDEO: Irene Uwoya kaamua kuweka wazi siri za urembo wa ngozi yake