Habari za Mastaa

Jina la Tekno limeondolewa kwenye list ya wasanii wanaowania tuzo za Headies

By

on

Yakiwa ni masaa machache yamebakia kufikia muda kutolewa tuzo za muziki nchini Nigeria zinazofahamika kama Headies, jina la star muimbaji wa muziki kutoka nchini humo Tekno Miles limeondolewa kwenye list ya wasanii wanaowania tuzo ya msanii anayechipukia baada ya Tekno kuikataa.imageHivi karibuni kupitia instagram yake, star wa huyo wa single ya Pana, aliandika maneno ya kuonesha kutofurahia kutajwa kwenye kipengele hicho kwa madai kwamba yeye sio msanii chipukizi kwasasa hivyo kumta kwenye category hiyo ni kumshusha na kumdharau.

Kupitia barua ya waandaaji, wamemjibu Tekno kuwa wamefanyia kazi maoni yake na hivyo kamati ya tuzo imeamua kuliondoa jina lake kwenye tuzo hizo na ikasainiwa na mtayarishaji mkuu kutoka Headies Ayo Animashaun.

Mr Eazi, Humblesmith, Ycee na Aramide ndio wasanii waliobaki kuwania tuzo hizo ambazo sherehe zake zinafanyika leo December 22, kwenye ukumbi wa Eko Convention Centre, Victoria Island, jijini Lagos Nigeria.

VIDEO: Full Performance ya TEKNO, Vanessa Mdee, Yemi Alade Alikiba, Barakah Da Prince na JUX kwenye jukwaa la FIESTA2016. Tazama video hii.

Soma na hizi

Tupia Comments