Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter>>>@millardayo na Zote nakusogezea hapa chini, Moja ya story kubwa June 04 2016 kwenye gazeti la Nipashe yenye kichwa cha habari ‘Msaidizi wa Kitwanga matatani bungeni‘.
Gazeti hilo limeripoti kuwa siku chache baada ya Rais John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani , Charles Kitwanga kutokana na ulevi, Naibu waziri wa Wizara hiyo, Hamad Yussuf Masauni, ameshtakiwa kwa uongozi wa bunge akidaiwa kutoa majibu ya dharau bungeni.
Nipashe limesema kwamba jana June 03 2016 mbunge wa Nkasi ‘CCM’, Ally Keissy alisimama na kuomba mwongozo wa Spika akidai Mhandisi Masauni amekuwa akitoa majibu ya dharau kwa wabunge.
Gazeti hilo limemnukuu Keissy kuwa alidai Naibu Waziri huyo amekuwa akitoa majibu ya kejeli na kiburi na kwamba wabunge wengi hawaridhishwi na majibu yake .
‘katika majibu ya msingi ya swali langu, wamesema serikali itakarabati majengo ya Kabwe, lakini anasema baadaye (kwenye swali la nyongeza) mbunge akarabati majengo ya Kabwe , si dharau hii?-Ally Keissy
‘hayo majibu yanaridhisha? anajibu kwa jeuri na kiburi, kusema kweli wabunge haturidhishwi na majibu ya Naibu Waziri, sikubaliani na majibu ya aina hii’:-Ally Keissy
#NIPASHE Naibu Waziri mambo ya ndani, Masauni ameshtakiwa kwa uongozi wa bunge akidaiwa kutoa majibu ya dharau pic.twitter.com/iFLPUfybBH
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#MWANANCHI Awamu ya pili mradi wa mabasi ya haraka unatarajiwa kuanza mwaka ujao wa fedha, itahusu barabara ya Kilwa pic.twitter.com/L58sHmR490
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#TanzaniaDAIMA Aliyekuwa waziri mambo ya ndani, Kitwanga amekwenda Israel kwa kile alichoeleza kulia na Mungu wake pic.twitter.com/BuvTKuuzIV
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#TanzaniaDAIMA Polisi DSM inamshikilia 'hausigeli' wa dada wa bilionea Msuya aliyetoroka siku moja kabla ya mauaji pic.twitter.com/ppfiS0DJb6
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#MWANANCHI Wabunge watatu CCM wamemkingia kifua Naibu Spika dhidi ya upinzani, wasema anaendesha vikao kwa kanuni pic.twitter.com/6LTOZ2Kl8t
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#MWANANCHI ACT Wazalendo wametangaza kufanya mkutano wa mapokezi kwa wabunge saba wa upinzani waliotimuliwa bungeni pic.twitter.com/HJYCNbOILB
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#NIPASHE Madereva wanaotanua barabarani hawatatozwa faini bali kuwekwa mahabusu na kufikishwa mahakamani pic.twitter.com/IZzzwMgYx6
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#NIPASHE Polisi Dar imeagiza wamiliki wa nyumba wawapige picha za kumbukumbu watu wanaopanga kwenye nyumba zao pic.twitter.com/GImo0JkBaR
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#NIPASHE Mil 100 zimetumika kutengeneza mabasi 34 ya UDART yaliyogongwa ktk kipindi cha chini ya mwezi mmoja pic.twitter.com/FX6A2VHk4H
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#NIPASHE Wabunge wa upinzani jana wametoka tena bungeni baada ya Naibu Spika, Tulia Ackson kuingia pic.twitter.com/3XFR9RoMxn
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
#MAJIRA Rais Shein asema hakuna kiongozi anayemuogopa Maalim Seif na atakayevunja sheria atahukumiwa kisheria pic.twitter.com/JNRLWpSRmJ
— millardayo (@millardayo) June 4, 2016
ULIKOSA HII YA WABUNGE WA CCM WAKIPINGA SHINIKIZO WAPINZANI KUTAKA KUMUONDOA NAIBU SPIKA DK TULIA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE