Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya story ambayo imeandikwa June 11 2016 kwenye gazeti la Mwananchi ni hii yenye kichwa cha habari ‘Mfugaji auza ngombe 3000, ajenga hospitali ya sh bil 2 Geita‘
Mfugaji Makoye Athuman, mkazi wa Mtaa wa Tambukara, kata ya Karanga mkoani Geita ameuza ng’ombe 3000 wenye thamani ya bil 2.1 na kujenga hospitali ya kisasa katika eneo hilo.
#MWANANCHI Mfugaji Geita ameuza ng'ombe 3,000 wenye thamani ya bil 2.1 na kujenga hospitali ya kisasa pic.twitter.com/jgM0HwWO2w
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
Gazeti hilo limeeleza kuwa mfugaji huyo maarufu kwa jina la Makoye Meno, alisema alichukua uamuzi huo baada ya kuguswa na ukosefu wa huduma za afya katika eneo hilo na aliamua kuwekeza kwenye sekta hiyo pamoja na kuondokana na migogoro ya wakulima na wafugaji. Athuman alisema hospitali hiyo itakuwa na wataalamu wa magonjwa mbalimbali na baadhi ya madaktari bingwa kutoka nchini India.
Waweza kuzipitia hapa nyingine kubwa kwenye magazeti ya leo June 11 2016
#NIPASHE Mkutano kwa ajili ya kumkabidhi uenyekiti CCM waota mbawa mwezi huu kutokana na ukosefu wa fedha za kuandaa pic.twitter.com/3jcKBol51I
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#NIPASHE Mbowe afungua kesi ya madai Mwanza kupinga amri ya polisi kuzuia mikutano ya vyama ya siasa nchini. pic.twitter.com/8HF52vjBrZ
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Sakata la Kitilya limetinga bungeni baada ya upinzani kuhoji sababu za baadhi kutofikishwa mahakamani pic.twitter.com/iYEvSxWx9M
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#NIPASHE TAKUKURU inakamilisha upelelezi wa kesi za vigogo ili kuanza nazo ktk mahakama maalum ya mafisadi pic.twitter.com/e32UVvsMnP
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Mpenzi wa mfanyakazi wa ndani mbaroni mauaji ya Aneth aliyeuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake pic.twitter.com/69JiSsdouy
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI TCRA yasema maandalizi ya mafunzo kwa watendaji kata, mitaa kuwatambua kitaalamu wakazi Dar yamekamilika pic.twitter.com/fLQvZ6kOxn
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Mahakama Kuu Dar imewaruhusu wanafunzi St Joseph kufungua kesi dhidi ya chuo na tume ya vyuo vikuu'TCU' pic.twitter.com/BAVI2IWnNh
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Imeelezwa kuwa Tanzania inaweza kufikia hali ya kutokuwa na maambukizi mapya ya Ukimwi ifikapo mwaka 2030 pic.twitter.com/MVx0GhrgcL
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Bajeti ya Kenya ni trilioni 50.6, ikiwa ni tofauti ya zaidi ya trilioni 20 kwa bajeti ya Tanzania pic.twitter.com/VnOodkwcdF
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#JamboLEO TPA imepanga kutumia zaidi ya bil 241.9 kujenga gati na matangi ya kuhifadhi mafuta kutoka Uganda pic.twitter.com/KLgQiStEvq
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#MWANANCHI Manispaa Ilala yamsaka chatu anayedaiwa kuishi karibu na mto Mzinga na kuwa tishio kwa wakazi wa Lubakaya pic.twitter.com/lRCjb6WKxx
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
#TanzaniaDAIMA Baada ya mahakama kuamuru faini mil 7 aliyemtukana Magufuli, marafiki, ndugu wamejitolea kumlipia pic.twitter.com/0QYiVgBw3r
— millardayo (@millardayo) June 11, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI JUNE 11 2016 KUTOKA AYO TV? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE