Michezo

KMC yamfyekelea mbali Jackson Mayanja

on

Baada ya kuwa na msimu wa kwanza mzuri katika Ligi Kuu ya Tanzania bara msimu wa 2018/2019 kiasi cha kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu, KMC msimu huu 2019/20 imekuwa ya kusuasua hali ambayo inatishia uhai wake wa kumaliza hata nafasi ya 10.

KMC inayomilikiwa na Manispaa ya Kinondoni leo asubuhi imetangaza maamuzi magumu ya kumfuta kazi kocha wao mkuu Mganda Jackson Mayanja kufuatia mfululizo wa matokeo yasioridhisha ya timu hiyo.

Maamuzi hayo yamefanyika kufuatia KMC kucheza mechi 8 za Ligi na kuonekana kusuasua, baada ya jana kufungwa game yao ya 4 ya msimu dhidi ya Kagera Sugar, ukizingatia wameshinda game 2 pekee na kutoka sare game mbili.

Mayanja anakuwa kocha wa tatu msimu huu kupoteza ajira yake baada ya Ndanda FC kufanya hivyo kwa kocha wao na Yanga kumfuta kazi kocha wao Mwinyi Zahera raia wa Congo, KMC sasa wapo nafasi ya 16 katika Ligi Kuu Tanzania bara wakiwa na point 8 tofauti ya point 4 tu dhidi ya Singida anayeshika mkia.

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

Soma na hizi

Tupia Comments