Fahamu kuwa Kanisa katoliki la Sagrada Familia lililopo Barcelona Hispania limeanza kujengwa toka mwaka 1882 huku likitarajiwa kumalizika kabisa mwaka 2032, mpaka sasa limetumia miaka 137 kujengwa na litakapomalizika ndio litakuwa miongoni mwa majengo yaliyotumia muda mrefu zaidi duniani kujengwa.
Mbunifu wa kanisa hilo Antoni Gaudi alikuwa anaamini kuwa haitakiwi kitu kilichotengenezwa na Mwanadamu kikawa kirefu kuliko kazi ya Mungu hivyo alilibuni jengo hilo ambalo likimalizika litakuwa na uwezo wa kuchukua Watu 9,000 huku minara yake ikiwa na urefu wa mita 170 ili liweze kuonekana katika kila pembe ya mji wa Barcelona.
Antoni Gaudi alijitahidi kulijenga kanisa hilo hadi kufikia robo na baadae alifariki mwaka 1926 na ndipo jengo hilo liliposimama na kuelezwa kuwa lilihitaji mchango wa fedha kutoka kwa watu ili likamilike. Iliripotiwa kuwa mwaka 2010 kanisa hilo lilifanikiwa kufikia nusu ya ukamilishaji huku miradi mingine ikiwa ni changamoto tokea mbunifu Gaudi afariki.
VIDEO: KIJANA ANAEMSAIDIA HAMIS KASIMULIA ILIVYOKUWA MPAKA AKAVIMBA MIGUU