Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema imefikia wakati mafuriko yawe ni fursa na isiwe laana kwani maji yake yanaweza kutumika katika utatuaji wa changamoto za maji ikiwemo katika Makao Makuu ya nchi Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Aweso amesema wizara ya maji itaangalia namna ya kuwekeza katika mabwawa ili maji ya mafuriko yaweze kutumika kwa kilimo cha Umwagiliaji na kwa Tanzania ya viwanda yanaweza kupelekwa kutatua changamoto ya maji Dodoma.
“Kikubwa ni miundombinu inatakiwa itengenezwe vizuri ili iwe rahisi kuvuna maji ya mvua na kuitunza rasilimali hiyo kwa sababu idadi ya watu imekuwa ikiongezeka na rasilimali zilizopo ni zile zile,“amesema.