Zaidi ya Pikipiki 100 zimekamatwa katika operesheni inayofahamika kwa jina la ‘hatutaki ajali’, iliyoendeshwa na Jeshi la Polisi usalama barabarani, Mkoa wa kipolisi Rufiji Wilaya ya Mkuranga.
Akizungumza Kamishina Msaidizi wa Polisi na Mkuu wa Usalama Barabarani, ACP Abdil Issango amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu ndani ya Wilaya ya Mkuranga, kibiti na Rufiji,kwaajili ya kuwakamata madereva wa pikipikiambao hawafuati na kutii kanuni na taratibu za usalama barabarani.
“Ajali nyingi ni bodaboda na kinachowaua ni mwendokasi, ukizingatia barabara zetu hazina miundombinu mizuri kwa kipindi hiki cha mvua, tutakachokifanya ni kuwakamata na kuwalipisha faini“ Kamanda Issango.
“Unapolipita gari jingine lazima uwe na uhakika unapopita, inawezekana kule unapopita miundombinu siyo mizuri hivyo unaporudi unaweza ukasababisha ajali“ Kamanda Issango.
“UMAMUITA BABY, HONEY HALAFU UNAMUUA KWA SHOKA, WIVU WA KIPUMBAVU” KAMANDA