Inadaiwa kuwa mtoto huyo alifariki nyumbani kwao kwa mshtuko baada ya kushambuliwa na kuku ambaye alikuwa anajaribu kulinda vifaranga vyake.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na tovuti ya The Standard, Mama wa mtoto huyo aitwaye Robai Toboko amesema, familia imebaki na majonzi kwa mtoto wake huyo wa miezi 6 kufariki akiwa mikononi mwake .
“Nilikuwa nimempakata mwanangu, katika ile harakati yake kujaribu kumkamata mmoja wa vifaranga, kuku huyo alimrukia mtoto kwa hasira na kumgonga usoni na bawa lake. Mtoto alishtuka na akaanza kulia kwa muda mrefu kisha akapoteza fahamu“ Mama wa mtoto
Aidha amesema mtoto wake alikuwa yupo vizuri kiafya ila alikata roho baada ya kupata mshtuko wa kushambuliwa na kuku, pia majirani walijitokeza kumsaidia japokuwa walikuwa wameshachelewa lakini walimuua kuku huyo pamoja na vifaranga vyake.