Leo January 11 2017 Baraza la Habari Tanzania ‘MCT’, kituo cha sheria na haki za binadamu ‘LHRC’ na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania ‘THRDC’ wamefungua kesi ya kuipinga sheria ya huduma ya vyombo vya habari namba 12 ya mwaka 2016, katika mahakama ya Afrika Mashariki ‘EACJ’.
Washirika hao wanataka baadhi ya vifungu vya sheria ambavyo vinakandamiza uhuru wa kujieleza vifutwe kwani vinakiuka matakwa ya mkataba wa jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo zinataka nchi mwanachama kuzingatia na kulinda haki ambazo zimeelezwa katika mkataba huo kwenye ibara 6(d) na 7(20).
VIDEO: Dakika 13 za Waziri Nape akisoma muswada wa huduma za habari, Bonyeza play hapa chini