Baada ya wabunge kupitia kamati ya hesabu za Serikali ‘PAC’ kufichua ufisadi kwenye shirika la taifa la hifadhi ya jamii ‘NSSF’ ambapo walibaini kuwa mradi wa NSSF wa kuendeleza mji wa kisasa wa Kigamboni jijini Dr es salaam ambao shirika hilo liliingia ubia na taasisi nyingine, thamani ya kila kiwanja kimoja iliyowekwa ni milioni 800 wakati thamani halisi ni milioni 25, hivyo kuwapo na malipo ya ziada ya mil 775 kwa kila kiwanja
Leo October 28 2016, msemaji wa Chama cha mapinduzi ‘CCM’ Christopher Ole Sendeka wakati akizungumza na waandishi wa habari ameligusia suala hilo na kuitaka Serikali ya Rais Dkt. Magufuli iendelee kukagua mashirika yote ya umma, wizara zote ili wale wote ambao wametumia fedha kinyume washughulikiwe.
Aidha Ole Sendeka amemshutumu Zitto Kabwe kwa kile alichosema amekuwa na chuki na serikali ya awamu ya tano, huku akidai alikuwa ni miongoni mwa viongozi waliokuwa wanasimamia shirika la NSSF hivyo anapaswa kuchunguzwa, Ole Sendeka amesema……..
>>>’chuki ya zitto kwa serikali ya awamu ya tano, akiinyooshea kidole kila kukicha wakati yeye alikuwa anasimamia mashirika hayo ambapo miongoni mwa taasisi hizo ambazo alikuwa anasimamia na baadhi ya marafiki zake ndio ambao wamenunua ekari moja kwa milioni 800 kumbe walikuwa wanajificha nyuma ya pazia kulikuwa na maslahi binafsi’
>>>’wakati umefika kwa serikali sio tu kuwashughulikia maafisa wanaoongoza taasisi hizi bali hata kuangalia akaunti za viongozi waliokuwa wakisimamia mashirika haya ambayo yameonyesha ufisadi mkubwa kuona kama akaunti hizo zinafafana na walichokuwa wanalipwa kutokana na mapayo yao halali’
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
Baada ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara, kutoa taarifa ya kusimama kwa mradi ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village, Kigamboni kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema wanahofia kupoteza Sh270 bilioni kutokana na kushirikiana na mbia ambaye hakuwa na fedha.
Profesa Kahyarara aliwaambia wajumbe wa PAC kuwa mradi wa Kigamboni ulisimama tangu Februari na kwamba juhudi zinafanyika kuhakikisha mbia huyo AHEL anarejesha fedha hizo.
Kwa muda sasa kumekuwepo na usambazaji wa taarifa za upotoshaji zinazotolewa na baadhi ya wanasiasa wakishirikiana na baadhi ya vyombo vya habari zinazolenga kukejeli, kudhihaki, kukatisha tamaa, kubeza na kudhoofisha jitihada zinazofanywa na Chama Cha Mapinduzi na Serikali zake katika kuleta maendeleo kwa Watanzania.