Habari za Mastaa

Mtandao unaosambaza mkanda wa Lil Wayne matatani, Wanasheria kuchukua hatua!

on

Wiki kadhaa zilizopita tulisikia kuwa kuna mtu anashikilia mkanda wa utupu wa Lil Wayne na amekusudia kuusambaza kwenye blogs na websites mbalimbali zinazopokea mikanda hiyo, wanasheria wa Lil Wayne wakasema itakuwa ngumu kwa yoyote kuuza mkanda huo bila idhini ya rapper mwenyewe, na kama ikitokea hivyo basi watachukua hatua kali dhidi ya mtandao huo… kuna mabadiliko yoyote?

WAYNEE4

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, mkanda wa utupu wa rapper Lil Wayne umeweka headlines kubwa sana baada ya mtandao wa HollywoodStreetKing kuanza kuachia vipande vya mkanda huo na kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, inaonekana Lil Wayne ameanza kukerwa na kitendo hiki.

WAYNEE2

Wanasheria wa Lil Wayne wameamua kuchukua hatua dhidi ya blog ya HollywoodStreetKing, kwa kuandika barua inayowaonya mtandao huo kuhusu kutumia video hiyo…

>>> “Mteja wetu anawataka muache kutumia videos mnazoziweka kwenye mtandano wenu mara moja, muache kusambaza nakala zozote za video hiyo, ikiwemo nakala za kielektroniki, pia mzifute nakala zozote zilizopo ili kutoendelea kuvunja haki zozote alizonazo mteja wetu Mr. Carter…” <<< ilisema moja ya sehemu ya barua hiyo.

 Team ya wanasheria ya Lil Wayne imewapa mtandao wa HollywoodStreetKing siku tano kuzifuta video zote za Lil Wayne kwenye mtandao wao… na kwa mujibu wa mmoja ya wanasheria wa Lil Wayne amesema kuwa mteja wake alikuwa hajui kama anarekodiwa hivyo asingependa kuendelea kuziona video hizo zikiendelea kusambaa.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments