NI WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mhe. Ummy Mwalimu ambae muda huu anazungumza na waandishi wa habari mwenendo wa ukusanyaji wa mapato kwenye kila Halmashauri.
Akizungumza katika mkutano huu wa waandishi wa habari muda huu anasema….”Kama ilivyoelezwa jana tulikuwa tutoe taarifa kuhusu ukusanyaji wa mapato wa Halmshauri pamoja na matumizi yake kwa mwaka wa fedha ambao umemalizi wa mwaka 2020/2021 na Mwaka Fedha kama mnavyofahamu wa Serikali unaanzia tarehe 1 July na kukamilika tarehe 30 June kwahiyo taarifa ninayotaka kutoa kwa watanzania kupitia kwenu wana habari ni kuanzia 1 July 2020 hadi tarehe 30 June 2021″– Ummy Mwalimu
“Kama mnavyofahamu ofisi ya Rais TAMISEMI ina utaratibu wa kutoa taarifa za ukusanyaji wa mapato wa ndani ya Halmashauri za Wilaya, Manispaa, na Majiji pamoja na matumizi ya mapato hayo kila robo Mwaka na lengo la hatua hii ni kuongeza uwazi na uajibikaji katika ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri”- Ummy Mwalimu
UNAWEZA UKABONYEZA PLAY KUSIKILIZA KINACHOZUNGUMZWA MUDA HUU NA UMMY MWALIMU