Staa wa NBA ambaye anachezea timu ya Cleveland Cavaliers kwenye ligi hiyo kubwa ya mpira wa kikapu Marekani, Lebron James ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa 20 kwenye orodha ya wachezaji waliofunga idadi kubwa ya pointi katika historia ya ligi hiyo.
James aliweka rekodi hiyo katika mchezo dhidi ya timu yake ya zamani ya Miami Heat ambapo alifunga jumla ya pointi 23 ambazo zilimfanya afikishe idadi ya pointi 24,816 katika kipindi cha miaka 11 ambayo amecheza kwenye ligi ya NBA.
Lebron amempita mchezaji wa zamani wa New York Knicks, Patrick Ewing ambaye alikuwa anashika nafasi ya 20 na inatarajiwa kuwa ataongeza idadi ya pointi hizi na labda kuingia katika orodha ya 10 bora na hata 5 bora kwa kuwa safari yake NBA bado inaendelea.
Hadi sasa Lebron amekuwa akiiongoza timu yake ya Cleveland Cavaliers kufanya vizuri kwenye msimu huu wa ligi ya NBA ambapo ameiongoza timu hiyo kufuzu hatua ya mtoano ya ligi hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipoondoka kwenye timu hiyo mwaka 2010.
Kaa karibu na millardayo.com, nitakachokipata nitakusogezea hapa muda wowote kuanzia sasa, unaweza kujiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>twitter Insta Facebook