Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro ameagiza vyombo vya dola kumkamata na kumhoji Mwenyekiti wa Mtaa wa Korongoni ambaye anadaiwa kuchangisha fedha kwa wananchi ili kugharamia mihtasari ya Kata kwenda Jiji ambayo kwa kawaida hutolewa bure.
DC Daqarro amesema Mwenyekiti huyo amekuwa anachangisha wananchi Tsh 50,000 kila mmoja akisema ni gharama za kufuatilia mihtasari Ofisi za Kata ambapo hadi sasa amechangisha wananchi 21 kati ya wananchi zaidi ya 65 ikiwa ni kinyume kwa sababu mihtasari hutolewa bure.
>>>”Kuna Mwenyekiti mmoja wa mtaa wa Korongoni anachangisha Wananchi 50,000 akisema ni gharama za kufuatilia mihtasari Ofisi za Kata. Mpaka sasa amechangisha Wananchi 21 kwenye zaidi ya Wananchi 65.
“Amefanya kinyume kwa sababu mihtasari haigharamiwi hutolewa bure…nimetoa maelekezo kwa vyombo vya dola wakamhoji. Hatuwezi kuruhusu viongozi ambao wametokana na wananchi, ambao wameajiriwa waendelee kutapeli wananchi wetu.” – DC Daqarro.
DC Arusha ameagiza M/kiti wa Korongoni akamatwe, anadaiwa kuchangisha fedha kugharamia mihtasari ya Kata inayotolewa bure #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/cxClJidMKU
— AyoTV (@ayotv_) September 3, 2017
Rais Magufuli atinga Kanisani kwa Wasabato Magomeni, awapa pesa
Rais Magufuli alivyokata tiketi na kupanda Pantoni…tazama kwenye hii video hapa chini!!!