Top Stories

Kiungo wa Tottenham Hotspurs Sisoko atua nchini

on

Kiungo wa Kimataifa wa timu ya soka ya Tottenham Hotspurs, Moussa Sisoko amewasili nchini leo June 15, 2019 kwa ajili ya mapumziko akiwa na mpenzi wake Marylou Sidibe.

Sisoko mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) majira ya saa 3:15 na ndege ya Shirika la ndege la Pression Air akitokea Nairobi nchini Kenya.

Akiwa katika uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) Sisoko alionekana mkononi akiwa ameshikilia box dogo la rangi ya blue likiwa na nembo ya timu ya Chelsea.

Kiungo huyo tegemezi wa Spurs anataraji kutemebelea vivutio vya Utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

MWANAFUNZI ALIYEONGOZA HKL NCHI NZIMA AZUNGUMZA, MMILIKI WA SHULE ATOBOA SIRI YA USHINDI

Soma na hizi

Tupia Comments