Leo October 2, 2019 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) imesema inafuatilia kwa ukaribu mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti na soko la Kisutu.
“Tutakamilisha ufatiliaji wa mradi wa ujenzi wa machinjio ya Vingunguti wenye thamani ya Tsh. Billion 12, kama mnavyofahamu mradi ule unafuatiliwa sana na sisi kama TAKUKURU tunaufatilia ili kuhakikisha hakuna uvujaji wa pesa za umma, pia tutaendelea kufanya ukaguzi soko la Kisutu” – Kamanda wa TAKUKURU Ilala, Christopher Myava.