Top Stories

Mambo Matatu yaliyozungumzwa na Familia ya MO DEWJI leo

on

Leo October 15, 2018 Familia ya Mfanyabisahara na mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji, imetangaza dau la Shilingi Bilioni 1 kwa atakayefanikisha kutoa taarifa za za kupatikana kwa mtoto wao.

Nukuu Tatu kubwa kutoka kwenye Press Confrence ya Familia ya MO Dewji

“Katika kuongeza juhudi za kuhakikisha Mtoto wetu mpendwa anapatikana Familia inatangaza zawadi nono ya Shilingi za Kitanzania BILIONI 1 kwa yoyote atakayetoa taarifa muhimu za kufanikisha kupatikana Mtoto wetu” -Familia ya MO DEWJI


“Familia inaahidi kwamba Mtoa taarifa pamoja na Taarifa vitabaki kuwa ni siri kubwa baina ya Mtoa taarifa na familia” -Familia ya MO DEWJI


“Siwezi kujibu maswali nawaomba muendelee kutuombea kuliko kutaka tujibu maswali” -Familia ya MO DEWJI

BREAKING: Familia ya MO Dewji yavunja ukimya yatangaza dau la BILIONI 1

Soma na hizi

Tupia Comments