Uzito wa Matukio mfululizo ya Migomo wa Madereva sio kitu kidogo, kila mtu aliathirika kwa upande wake… haikuwa kitu ambacho Serikali ilikiacha kikaendelea.
Kulikuwa na madai mengi ambayo Madereva walihitaji Serikali iingilie kati… kwenye Madai yao iko ishu ya Madereva kufanya kazi pasipo kuwa na Mikataba, Sheria ya kuwalazimisha warudi Vyuoni kusomea Udereva kila baada ya muda fulani kupita, na mengine.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni DC Paul Makonda hakuliacha hilo, baada ya kuyasikiliza madai ya Madereva aliingilia kati na kuanza kushughulikia madai hayo.
October 03 2015 inaingia kwenye Kumbukumbu ya Umoja wa Madereva, kwa mara ya kwanza wamekutana na Rais Jakaya Kikwete na kuyafikisha madai yao kwake moja kwa moja.
Kutoka Ubungo PLAZA Dar sasahivi nakusogezea #TWEETS kila kinachoendelea, Rais JK amekutana na Umoja wa Madereva wa TZ-#MillardaAyoUPDATES
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Serikali inajenga barabara kwa ajili ya madereva, madereva ni muhimu kwenye Uchumi wa nchi’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Nampongeza DC Paul MAKONDA kwa jitihada zake kumaliza mgomo, japo wengine walikuwa wakishangilia migomo’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Madereva wameelezea Changamoto zao, nimezielewa. Mambo yote ni ya msingi, yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi’-#RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Nawapongeza Madereva kwa kuunda Chama chao, ni jambo jema. Mkiwa na umoja mnajenga nguvu ya kuongelea’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Nilisikitika kusikia Madereva wanafanya kazi bila Mikataba,Dereva anakosa haki za Msingi kwa kukosa Mkataba’-#RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Kundi la watu ambao hawalipwi vizuri, Serikali inawasaidia kwa kuwasikiliza wao na waajiri wao’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Mgogoro wa Madereva uko mikononi mwa SUMATRA, mkitimiza Wajibu wenu hakuna mgogoro”- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘DC Makonda kajitolea kufanya kazi ya kumaliza mgogoro wa Madereva, ilikuwa kazi ya SUMATRA”- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
“Nataka SUMATRA waniandalie majibu kuhusu Mishahara ya Madereva, Posho na Mikataba yao”- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘SUMATRA wanatakiwa kusimamia mazungumzo na muafaka wa Madai ya Madereva upatikane’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Madereva wanalalamikia kudaiwa ‘kitu kidogo’ na Askari wa Usalama Barabarani, Kamanda MPINGA atusaidie hili’-#RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Tukipunguza wanaodai ‘kitu kidogo’ barabarani maisha ya madereva yatakuwa vizuri’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
Ajali ni nyingi sana, watu wanafariki na mali zinapotea kwa sababu Madereva wengi hawazingatii Sheria”- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Madereva wakizingatia Sheria za Usalama Barabarani hata Tochi hazitokuwepo’- #RaisJK #MillardAyoLIVEUpdates #MaderevaTZ — millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
‘Nitashughulikia madai ya Madereva, baada ya Mazungumzo tutapata Muafaka wa Madai yote’- #RaisJK#MillardAyoLIVEUpdates#MaderevaTZ
— millard ayo (@millardayo) October 3, 2015
Baada ya hapo Rais JK alipita kuagana na Madereva pamoja na kupiga picha za pamoja kwa ajili ya Kumbukumbu ya tukio la leo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? Kama unatumia Mtandao wa tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTERFBYOUTUBE