Kama na wewe ni miongoni mwa walioziona lakini ukatamani kupata maelezo yake kama wengine wengi, tumempigia simu Ommy Dimpoz ikiwa ni saa zaidi ya 9 toka picha hizi ziwekwa Instagram na amesema tunachotakiwa kufahamu.
Dimpoz amesema picha hizi sio za mapenzi bali wako kazini na hapa ni Mombasa Kenya kwenye scene ya video yake mpya ambapo mara ya mwisho kumuona Ommy Dimpoz kafanya ngoma na Msanii wa kike Tanzania ilikua zaidi ya maka mitano iliyopita alipoidondosha ‘me and you’ ft. Vanessa Mdee, sasa hivi katisha na Nandy.
Sasa leo tunajua Ommy ka-trend na picha zake na Nandy, ukweli ni kwamba picha hizo zinatoka kwenye scenes za goma lake jipya ft. Nandy ambalo linadondoshwa siku yoyote wiki hii, hayo ndio maelezo ya Dimpoz baada ya kupost hizi picha bila maelezo ya kutosha kwenye Instagram ambapo aliandika tu Happy New Year.
Dimpoz ameiambia millardayo.com kwamba mikono ya Producer Yogo imehusika kwenye ngoma hiyo ambayo pia ndio ya kwanza kufanya na Nandy, malizana na subscription mapema hii kwenye Youtube ya Ommy.
EXCLUSIVE: “SUMU NDIO CHANZO CHA MIMI KUUMWA”