magari

Njia tano zitakazokuwezesha kutumia simu wakati unaendesha gari

on

Naamini utakuwa unajua namna ajali mbalimbali za barabarani zinavyochukua headlines miaka ya hivi karibuni ambapo miongoni mwa sababu zinazotajwa ni kutozingatia kanuni na sheria za usalama barabarani.

Kwa usalama hairuhusiwi kuongea na simu wakati unaendesha gari ambapo zimewekwa faini mbalimbali kwa atakayekamatwa na kosa hilo hivyo ili kuepusha ajali zitakazogharimu maisha ya watu makampuni kadhaa ya magari ya kisasa yamekuwa yakijitahidi sana kuona namna gani mtu anaweza kutumia simu yake wakati anaendesha gari.

March 17, 2017, nakusogezea njia 5 zitakazokusaidia kutumia simu kwa namna yoyote uipendayo wakati unaendesha gari yako.

5: Kutumia Bluetooth

Magari ya kisasa siku hizi yanawekwa Bluetooth ambayo inakuwezesha kuunganisha simu yako na mfumo mzima wa media katika gari yako. Unachotakiwa kufanya ni kuunganisha simu yako na magari yenye uwezo wa namna hiyo utaweza kuendelea kuitumia simu yako wakati unaendesha.

4: Kutumia application ya Siri/GoogleNow

Teknolojia imepevuka – sasa unaweza kufungua apps, kufungua music, kutuma emails na mengi zaidi kutumia sauti yako. Siri na GoogleNow ni njia mbili salama kuitumia simu yako wakati unaendesha. Hii inapatikana katika baadhi ya magari ya kisasa au simu za iPhone na Android.

3: Kutumia Built-in SIM

Yapo magari kwa maendeleo ya Teknolojia siku hizi yametengenezwa na simu (yana simu moja kwa moja). BMW, kwa mfano, yana sehemu ambayo huwekwa SIM card ambayo huwezesha matumizi mengi (baadhi yao huwa na uwezo wa smartphones).

2: Kutumia Apple Carplay/Android Auto

Ni kitu ambacho kinafanya vizuri sana sokoni siku hizi. Hii ni huduma iliyojengwa kwenye mifumo ya taarifa na burudani, lakini pia inaweza kuwekwa kwenye gari yako kama siyo ya kisasa. Apple na Android wametengeneza software ambayo inaiwezesha simu yako kuunganishwa kwenye gari.

1: Simama

Pindi unapopigiwa simu, njia salama na ya busara (iliyo halali) kutumia simu yako ukiwa unaendesha ni kusimamisha gari yako na kufanya chochote upendacho. Hakuna siri kuwa ajali hutokea na maisha hupotea kwa watu wanaotumia simu wakati wanaendesha magari.

AyoTV MAGAZETI: Ulizikosa story kubwa zilizoandikwa kwenye magazeti ya March 7 2017? Bonyeza play hapa chini kutazama.

Unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments