Kama hukuwa karibu na Redio yako na ukashindwa kusikiliza uchambuzi wa Magazeti yakisomwa na kuchambuliwa hewani kupitia Power Breakfast ya Clouds FM leo February 12, nimekurekodia unaweza kuyasikiliza hapa mtu wangu.
Miongoni mwa Habari zilizopo kwenye Magazeti ya leo ni pamoja na ile inayosema kivuko cha Mv Dar kinatarajiwa kuanza kazi wakati wowote kuanzia sasa, Mwanasheria Mkuu amesema vikundi vya ulinzi vilivyoanzishwa na vyama vya siasa nchini ni haramu, raia wa Ubelgij akamatwa na fuvu la binadamu Dar, Takukuru imekiri kuwepo kwa baadhi ya watumishi wake wanaojihusisha na masuala ya rushwa, watumiaji wa dawa za ARV wako hatarini kutokana na kuingizwa sokoni dawa zisizo na ubora na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameshauri kushuka kwa bei ya mafuta kuendane na vitu vyote vinavyotumia nishati hiyo.
Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ambae amezungumzia swala la kushuka kwa bei ya mafuta na kuiomba SUMATRA kutangaza bei mpya za usafiri ili mwananchi wa hali ya chini aweze kufikiwa na unafuu huu.
88.0 Clouds FM inasikika ukiwa Tabora.
Bonyeza play kusikiliza Uchambuzi wa Magazeti ya Leo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook