Magazeti ya leo tayari yapo mtaani, POWERBREAKFAST ya Clouds FM imefanya uchambuzi wa story kubwa zote za kwenye kurasa za Magazeti Tz, kama ulikuwa mbali na radio yako basi hapa unaweza kusoma na kusikiliza stori zote.
Kwenye Magazeti kuna hizi leo; Ofisi ya Bunge imesema haijapata barua kuhusu kuvuliwa ubunge kwa Zitto Kabwe, Mlinzi wa Dr. Slaa amesema hahusiki na njama zozote za kumuua Dk.Wilbroad Slaa, Jaji Mkuu Tz Mohamed Chande amevitaka vyombo vya dola kujipanga kushughulikia kesi za mauaji ya albino.
Jeshi la Polisi limewakamata wapiga ramli 225 Tz, Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi ajali ya basi na lori iliyoua watu 42 Iringa, hukumu ya aliyekuwa Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka kuhusu mgawo wa fedha za ESCROW inatarajiwa kutolewa kesho na kuna story kutoka Kenya inayohusu wanawake kuishi kwa mashaka kutokana na nyani wanaovamia mashamba yao kutaka kuwabaka.
104.1 Clouds FM inasikika ukiwa Bukoba.
Bonyeza play hapa chini kusikiliza story zote…
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook