Asubuhi siku zote huanza na uchambuzi wa magazeti @CloudsFM The Peoples Station, na pengine sio zote zimekufikia, unaweza ukacheki na hizi kubwa nyingine kufidia.
Maelfu wakanyagana Tanga kutaka kumuona Lowassa, Dk Magufuli na Nape Nnauye waishangaa CHADEMA, Magufuli asema haiwezekani wachache kula kuku kwa mrija… Mahujaji 50 wapotea Mecca, Nape Nnauye amlipuwa Lowassa.
Mgombea Urais wa CHADEMA Edward Lowassa avunja mkutano Tanga kwa hofu ya watu kukanyagana na kupoteza maisha baada ya mafuriko ya watu kuzidi kupita kiasi kwenye uwanja wa Tangamano, Dk John Magufuli asema amejipanga kulipa deni kwa Watanzania kwa kuleta maendeleo ya kweli na Serikali yake ya awamu ya tano itakayo toa fursa kwa Watanzania kufaidi rasilimali za nchi yao.
Mahujaji 5 kutoka Tanzania wafariki Saudi Arabia huku wengine 50 hawajulikani walipo, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa binadamu NIMR imetoa tahadhari kwa mlipuko wa magonjwa yatakayotokana na mvua za El Nino mwezi October na December, baadhi ya magonjwa yakiwa ugonjwa wa bonde la ufa na robo tatu ya Watanzania wamebainika kuwa na matatizo ya moyo huku 26% wakiwa na uzito uliokithiri.
Mgombea Urais kupitia Chama cha CHAUMMA Hashim Rungwe asema iwapo atachaguliwa kwenye uchaguzi mkuu October 25 ataunda Baraza dogo la Mawaziri wasiozidi 20, asema ataunganisha Wizara zenye majukumu yanayofanana kuwa Wizara moja.
Sauti ya uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast ipo hapa chini, bonyeza play kusikiliza.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa, muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata, pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> YouTUBE