Mathias Ernest mwenye miaka 32 alipata ajali akiwa njiani kwenda Burundi akifanya kazi ya udereva wa magari makubwa kusafirisha ngano kutoka Tanzania kwenda Burundi taarifa za awali zilisema amepoteza maisha ndugu wakaweka msiba nyumbani kwao, baadae zilitoka taarifa kuwa ni mzima japo hali yake sio nzuri, alipatiwa matibabu Hospitali ya Bugando Mwanza kwa muda wa miezi miwili na baadae kuruhusiwa.
kwa sasa Mathias hawezi kusimama wala kutembea ameuza nyumba yake ili aende India kwa matibabu zaidi lakini pesa haijatosha.