Wataalam wa Urusi katika maabara ya Sensor-Tekh wamefanikiwa katika majaribio ya kifaa ambacho kinawezesha vipofu kuweza kuona.
Kifaa hicho kilichopewa jina la ELVIS (ELectronic VISion) kina sehemu mbili, headband ya kuvaa na implant. Headband inavaliwa na unaweza kutolewa, na implant ni kifaa kidogo ambacho kinawekwa karibu na sehemu ya Cerebral Cortex kwa kuunganisha Electrones zake na cortex kwa njia ya upasuaji. Kinawekwa sehemu ya ubongo inayohusikana na kuona.
Baada ya kuwekewa kifaa hicho, mgonjwa anatembea na headband yenye kamera, ambapo headband hiyo imekaa kama mkanda wenye kamera ambazo zinawekwa mbele na kutazama kama macho. Headband hiyo inatuma signal za picture moja kwa moja kwenye implant, na implant inatafsiri mawimbi kuwa picha katika ubongo.
Changamoto ambayo wataalam wanapambana nayo, Kifaa kinachowekwa katika cortex kinatakiwa kubadilishwa kila baada ya miaka 10. Na kinafaa kwa mtu mwenye miaka 24 mpaka 65 kutokana na hali ya cortex yake kuwa rahisi kuunganishwa na kifaa hicho.
Kifaa hicho kinamwezesha kipofu kuona vizuri, japo rangi hazionekani vizuri sana kama mtu wa kawaida; lakini kipofu ataweza kutembea, kuona watu na vitu vizuri kwa urahisi.
Wiki hii teknolojia hii imeonyesha mafanikio, ni teknolojia kubwa ya kusaidia vipofu na inategemewa mwaka 2023 itaanza rasmi kuwekwa kwa watu ambao watajitolea.