Kampuni ya Acacia inaondolewa katika orodha ya kampuni zilizopo kwenye soko la hisa la Dar es salaam (DSE) kuanzia leo, Novemba 18, 2019.
Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam Emmanuel Nyalali, amesema kampuni hiyo ambayo imedumu katika soko hilo kwa miaka 8 ikiorodheshwa tangu Desemba 2011, ilifutwa katika Soko la Hisa la London Uingereza (LSEG) tangu September mwaka huu, hivyo utaratibu wote umefuatwa.