Wananchi wa kata ya Terati mkoani Arusha wameiomba serikali kuwasaidia kurekebisha miundombinu ya daraja la barabara ya Afrika Mashariki,baada ya mkondo wa maji kuelekezewa kwenye makazi ya watu nakupelekea nyumba kujaa maji huku wengine wakishindwa kupita na barabara kuharibika.
Daudi Mollel mwenyekiti wa mtaa Olkong amesema maji hayo ni ya muda mrefu kutokana nakukosekana kwa mkondo wa maji nakusababisha maji kuelekea kwenye makazi ya watu.
“Maji yameingia huku ndani wengine jana usiku hatujalala tunafanya kazi yakutoa maji ndani saa nyingine baba amelala hawezi kuamka ahangaike na maji akina mama sisi ndio tunateseka”-Shakila Yahya mkazi wa Terati