Waziri wa nchi ya ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na mazingira January Makamba ameanza ziara mikoa ya Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida yenye lengo la kutambua changamoto za kimazingira na kuweka mikakati sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri Makamba ameanza ziara hiyo mkoani Pwani kwa kutembelea na kukagua changamoto za kimazingira katika halmashauri za Bagamoyo na Chalinze huku akitarajiwa kuendelea katika mkoa wa Tanga.
Katika Wilaya ya Bagamoyo Waziri ametembelea na kukagua eneo la Mto Mpiji unaotenganisha mkoa wa Dar es Salaam na Pwani eneo la Kata ya Mapinga kitongoji cha Kibosha ambapo amekagua shughuli za utunzaji mto huo ambao unakabiliwa na changamoto kubwa ya uchimbaji wa mchanga kwaajili ya shughuli za kibinadamu ikiwemo mahitaji ya ujenzi.
VIDEO: Ziara ya January Makamba, ni yeye na Mwananchi mmojammoja, Bonyeza play hapa chini kutazama