Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameagiza kutafutwa popote alipo na kumkamata Mama mmoja aliyetajwa kwa jina la Atuganile Kalenge, ambaye anatuhumiwa kuwatapeli wananchi kwa kuwauzia viwanja na nyumba katika eneo la Gombe Kusini Jijini Mbeya na kwenda hadi Ikulu Jijini Dar es salaam ambako amemdanganya Rais Dk. John Magufuli kuwa anatishiwa kuuawa na pia hana imani na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya.