Mgombea nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
“Nasema ahsanteni sana, na huo ni ujumbe tosha kwa wale wanaojitokezatokeza, wataisoma namba” Rais Magufuli
“Na kilichonifurahisha zaidi, wananchi waliohudhurua hapa, pamoja na waliojaa nje, si wanaCCM tu, ni wa vyama vyote kwa sababu wanaamini katika maendeleo na maendeleo hayana chama” Rais Magufuli
“Katika kipindi kifupi cha miaka mitano, Tanzania imevuka kwenye level ya nchi maskini na kuwa nchi ya uchumi wa kati, nipeni tena miaka mitano sijui tutaenda kwenye uchumi wa katikati” Rais Magufuli
“Hakuna nchi yoyote ambayo imevunja uhusiano na TZ hii ni kudhihirisha katika kipindi cha miaka 5 tumefanya vizuri katika masuala ya kidplomasia, na tumetembelewa na viongozi wa nchi na Taasisi mbalimbali” Rais Magufuli
“Wengine watasema yatampigia kura Madaraja na Mabarabara hayo anayoyachagua, kwani hayo mabarabara hawapiti watu, basi watu wanaopita kwenye madaraja hayo naomba mnipigie kura” Rais Magufuli
“Na ndiyo maana uwanja wa hapa Mwanza tumeupanua Ndege yoyote ya Duniani itatua hapa, wakishatua hapa mwenye guest hujapata watu, anayetafuta mchumba Mzungu hajampata?, anayetaka kumsindikiza Serengeti hajapata wa kumsindikiza?” Rais Magufuli
“Katika mipango ya baadaye tunarasimisha hizo nyumba zilizopo huko juu, hakuna mtu akayebomolewa nyumba yake kule juu, Serikali itapeleka huduma zake kule kule juu, kaeni kwa raha kwanza milimani ndiko kwenye hewa nzuri ya kuvuta” Rais Magufuli
“Tumeanza kujenga Reli ya umeme, mtu unatoka hapa Mwanza kwenda DSM kwa masaa 8, ili kusudi ikamilike ndiyo maana tumekuja tena kuwaomba kura, inawezekana mkachagua wengine tutakuwa tumepoteza mipango ya kuiendeleza Mwanza” Rais Magufuli
“Katika historia yangu katika miaka ya 1978 nilisomea hapa, nilikuwa natokea Igogo napita Bugando, nateremkia Mwanza Sec ninakuja Rufiji ninatokea Mtaa wa Azimio nakuja Lake kusoma, asubuhi na jioni nilikuwa natembea kwa mguu” Rais Magufuli
MAGUFULI AMVULIA DIAMOND KOFIA, AMUITA MEZA KUU AMSHIKA MKONO