Leo February 8, 2019 Mwenyekiti wa Bodi ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji maarufu MO amezungumza na Waandishi wa habari Ofisini kwake juu ya maendeleo ya Klabu hiyo na kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali, hapa nakusogezea mambo matano makubwa alioyaongea MO.
Jambo la kwanza ni MO ametoa pole kwa Wanasimba >>> “Nianze kutoa pole kwa Wanasimba na Wanasoka wa Watanzania kwenye mechi hizi mbili Simba tumepita kwenye wakati mgumu sana, tumeshindwa kwa magoli matano” MO Dewji
Jambo la pili ni ukubwa wa Klabu ya Al Alhly iliyowafunga tano “Ukiongelea Al Ahly unaweza kuilinganisha na Real Madrid kwenye mataji, juzi wamenunua mchezaji kwa zaidi ya Bilioni 10 na huyo mchezaji ametoa assist zaidi ya tatu kwenye mechi tuliocheza nao” MO Dewji
Jambo la tatu ni kwenye mpira hamna njia ya mkato “Kwenye mpira huwezi kuchukua lift upande juu lazima upande ngazi, nawaomba Wanasimba tusivunjike moyo wote tumeumia, huo ndo mpira, Mi naona tuna nafasi, tulishawahi kuwafunga Al Alhly hapa nyumbani” MO Dewji
Jambo la nne ni hamasa katika vitu ambavyo mtu unataka kufanya kutokata tamaa “Hakuna mtu Duniani ambaye hajawahi kushindwa hakuna mtu, unaweza usifanye vizuri kwenye Mitihani lakini sio kwamba hautafanikiwa” MO Dewji
Na jambo la tano ni kuhusu pesa “Pesa ni muhimu lakini money is not everything” MO Dewji