Michezo

Tazama mabao ya mchezo wa fainali ya Capital 1 kati ya Man City vs Sunderland

on

article-2570381-1BF7AFFF00000578-312_634x431Mabao yaliyofungwa na Yaya Toure, Samir Nasri na Jesus Navas dhidi ya Sunderland katika mchezo wa fainali ya kombe la Capital One yameipa klabu hiyo ya jiji la Manchester ubingwa wa kwanza msimu huu.

Sunderland walikuwa wa kwanza kuliona lango la Man City katika dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza kupitia mshambuliaji Fabio Borini, bao lilodumu mpaka kipindi cha pili. City wakarudi kwa kasi na kusawazisha kupitia Toure  kabla ya Samir Nasri na Jesus Navas kumaliza na kuipa timu yao ubingwa wa kwanza chini ya mwalimu Manuel Pellegrini.

Tupia Comments