Usiku wa kuamkia July 26 vilabu viwili vikubwa barani Ulaya vilikutana kucheza mchezo wa International Champions Cup, michuano ambayo bado inaendelea katika nchi mbalimbali na sehemu zingine kumalizika…Michuano hii ambayo klabu nyingi hutumia kama sehemu ya maandalizi ya msimu mpya ya Ligi Kuu katika nchi zao, usiku wa July 25 kuamkia July 26 umezikutanisha timu za FC Barcelona ya Hispania dhidi ya Manchester United ya Uingereza.
Mchezo huo umepigwa katika Uwanja wa Levi’s Stadium California Marekani hadi dakika 90 zinamalizika Manchester United imeibuka na ushindi wa goli 3-1 magoli yakifungwa na Wayne Rooney dakika ya 8, Jesse Lingard dakika ya 65 na Adnan Januzaj dakika ya 91 huku goli pekee la kufutia machozi kwa FC Barcelona likifungwa na Rafael Rafinha dakika ya 90.
Hii sio mara ya kwanza kwa klabu za FC Barcelona na Manchester United kucheza mechi ya kirafiki kama hiyo ya International Champions Cup 2015, kwani iliwahi kukutana mwaka 2011 na Man United kuibuka mshindi kwa goli 2-1 kabla ya mwaka 2012 kukutana tena na FC Barcelona kushinda kwa mikwaju ya penati.
https://youtu.be/nB1E3jOnM1k
Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.