Stori Kubwa

Baada ya Headlines za Kenya, bibi mwingine karudi darasani akiwa mzee kabisa Marekani..

on

marie

Elimu haina mwisho! Unaikumbuka ile stori ya bibi wa Kenya mwenye miaka 90 ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi akiwa darasa la tano na watoto wadogo ambao ni sawa na wajukuu zake Kenya?

Nna hii nyingine toka Marekani, bibi anaitwa Marie Hunt.. yeye nd’o ametoka kuhitimu masomo ya ngazi ya Diploma,  River Valley High School huku akiwa na umri wa miaka 103.

Marie angeweza kuhitimu elimu hiyo miaka 87 iliyopita lakini haikuwa hivyo kutokana na sababu mbalimbali

Marie anayeishi Wisconsin, Marekani amesema sababu kubwa iliyomfanya kushindwa kuendelea na masomo wakati akiwa mdogo ni kukosa fedha na pia kuwa na jukumu la kuwaangalia wadogo zake.

Hunt alitakiwa kumaliza masomo mwaka 1928… alitamani siu moja kutimiza ndoto zake za kusoma na sasa amehitimu Diploma katika shule  River Valley High School.

Bado haijafahamika kama ataendelea na masomo zaidi lakini amesema anatamani kuwa mmoja wa wahitimu wa chuo kikuu.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter, instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments