Serikali imeagiza Kaya 13 zilizopo eneo la wafugaji katika Hifadhi ya Wembele Wilayani Igunga Mkoani Tabora kuondoka katika eneo hilo kwenda eneo ililopangiwa la wakulima ili kuondoa mgogoro wa muda mrefu kati ya wafugaji na wakulima.
Kauli hiyo ya serikali inafuatia wakulima kuvamia eneo la wafugaji katika kijiji hicho na kuzuia wafugaji kulisha mifugo yao jambo lililokiuka makubaliano ya awali ya kila upande kubaki katika eneo lake kwa ajili ya shughuli zake.
‘’Waliokiuka utaratibu wa awali waondoke, ziko kaya 13 hatuwezi kuendelea na vifo katika haya, serikali ishaweka mipaka kinachotakiwa ni kuheshimu maamuzi’’ Mabula
“UGUMU WA MAISHA NIKAAMBUKIZWA UKIMWI GEREZANI, NASUBIRI KIFO, NDUGU WOTE WAMEFARIKI”