Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo akiwa katika ziara ya kukagua mwenendo wa mradi wa maji ya Ziwa Victoria Mkoani Tabora amewataka Wananchi kutunza vyanzo vya maji wakati Serikali ikifanya jitihada za kutatua uhaba uliopo kulingana na ongezeko la watu.
“Ziwa Victoria lipo Tanzania kwa 50% tunatumi maji 0.011%, kila Mtanzania ukimgawia maji angepata mapipa 9000, kitakwimu Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na maji sisi tupo mita za ujazo 1800 wakati tunapata uhuru kila mtu angepata mita za ujazo zaidi 7000 tunaongezeka lakini maji hayaongezeki” Prof. Kitila