AyoTV

Habari mpya kuhusu Dogo Mfaume…alirekodi wimbo kabla ya kifo

on

Siku mbili tangu aliyekuwa mwimbaji wa Mchiriku Dogo Mfaume afariki akisubiri matibabu Hospitali ya Muhimbili, story ambayo inasambaa kwenye mitandano ya kijamii kwa sasa ni kuhusu kufanya wimbo mpya ambao alitaka kuutoa kupitia WCB.

Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Mkurugenzi wa Sober House Pili Misana amefunguka na kusema kuwa kabla ya kufariki May 17, 2017 Dogo Mfaume alirekodi wimbo mpya unaoitwa Baba Mkwe ambapo kulikuwa na mipango ya kuupeleka Wasafi ili waitambulishe media mbalimbali.

“Mara ya mwisho tulirekodi wimbo mpya unaoitwa Baba Mkwe ambapo nilikuwa nishazungumza na Babu Tale niipeleke pale Wasafi. Bahati mbaya ndio hivyo akaanza kuumwa, akazidiwa. Kwa hiyo nikawa nimeshindwa kwenda lakini Babu Tale alishasema tuupeleke ili waitambulishe kwenye Media mbalimbali.

“Kwa hiyo, wimbo ninao na naweza kusema ndio kumbukumbu aliyoniachia na nikiusikiliza namuona Dogo Mfaume mpya kabisa ambaye ana uchungu na kazi yake. Alikuwa ameshaimba wimbo wa Dawa za kulevya kuhamasisha watu waache kutumia dawa hizo.” – Pili Misana.

BAADA YA KIFO: Man Water kaelezea ‘Kazi ya Dukani’, alivyokutana na Dogo Mfaume

Soma na hizi

Tupia Comments