Moja ya headline kutokea Dodoma ni kamati ya madiwani kushinikiza kuondolewa kwa Mstahiki Meya wa manispaa hiyo Jafary Mwanyemba anayetuhumiwa kwa hujma mbalimbali ikiwemo kugushi nyalaka feki na kujipatia zaidi ya shilingi Milioni 30.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi amesema>> ‘Moja ya hoja iliyofikishwa kwangu ni ubadhirifu wa mradi wa maji katika kata ya Zuzu uliokuwa umefadhiliwa na Ubalozi wa Japan ambapo zilitolewa takrimani milion 122 kwa ajili ya kutatua tatizo la maji‘
‘Kulikuwa na mapungufu makubwa wakati wa utoaji wa zabuni, kitu ambacho kinasababisha Meya wa manispaa ya Dodoma aonekane anahusika ni kutokana na mazingira ya utoaji huo ambapo kwanza mkataba ulisainiwa tarehe 14 mwezi wa nne kisha kikao kikafanyika tarehe 28 mwezi wa nne‘ –Godwin Kunambi
‘Hili ni kosa la kisheria kwasababu kikao ndio kinatakiwa kianze kupitisha zabuni kabla ya mkataba kusainiwa, baada ya hili jambo kufikishwa Polisi na baada ya uchunguzi ikabainika kuna pesa zimegushiwa ndipo mkandarasi akakamatwa na akawataja watu waliompa pesa akiwemo Meya wa Dodoma‘ –Godwin Kunambi
‘Na kuthibitisha kwamba Mstahiki Meya anahusika ni kitendo cha yeye kuja na kurudisha fedha baada ya Polisi kumsumbua, kama kweli hakuhusika kwenye wizi wa hizo fedha zaidi ya Milioni 30 ilikuwaje aje kuomba kuzirejesha?‘ –Godwin Kunambi
Unaweza kuendelea kumsikiliza Mkurugenzi Godwin Kunambi akielezea mambo yote yalivyokuwa kwenye hii video hapa chini….
VIDEO: MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU KUHUSU KUKAMATWA KWA FREEMAN MBOWE
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo