Headlines za leo kutoka Africa zinaandikwa na Bakary Yerima Bouba Alioum Mfalme kutoka Bafut, Kaskasini mwa Cameroon… Bafut ni moja ya sehemu ambazo ziko ndani ya Cameroon ziko chini ya utawala wa Kichifu.
Bakary Yerima Bouba Alioum ni Mfalme wa kumi na moja wa Bafut aliyevaa majukumu ya Ufalme akiwa na miaka 16 baada ya baba yake aliyekuwa Mfalme kufariki mwaka 1968, amekuwa mfalme kwa zaidi ya miaka 47 sasahivi.
Mfalme Bakary ana kitu kingine kikubwa ambacho kimefanya awe story leo, ana wake 100 na watoto zaidi ya 500… Kwenye moja ya Interview aliwahi kufanyiwa, ameelezea sababu za yeye kuwa na wake wengi na watoto wote hao.
>>> “Wake hawa wote hawakuwa wangu kuanza nao, nina wake watatu ambao nimewaoa.. hawa wengine wote nimewarithi baada ya baba yangu kufariki, wengine na yeye aliwarithi baada ya babu yangu kufariki. Kimila, Mfalme akifariki anayefuata kiuongozi anarithi wake zake wote.” >>> Mfalme Bakary.
>>> “Mila zetu zinasema, ukiwa Mfalme wale wake wote wakubwa waliotangulia wana jukumu la kumfundisha Mfalme mila na tamaduni hizi kwani Mfalme anakuwa bado hajukua kuwa Mfalme” >>>
>>> “Malkia kwenye himaya hii wanachukua nafasi kubwa sana, wanawake hawa wanatakiwa kumjenga Mfalme wao ili aweze kuyamudu majukumu yake kama Mfalme na pia kama mwanaume” >>>Mfalme Bakar.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.