Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kwa hatua madhubuti za kufanya mageuzi ya kiuchumi katika nchi hiyo na ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe.
Rais Magufuli amesema hayo wakati akitoa hotuba katika dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Rais Mnangagwa kwa heshima yake na kufanyika Ikulu Jijini Harare.
Rais Magufuli amesema katika kipindi kifupi cha tangu Rais Mnangagwa aingie madarakani hali ya uchumi imeanza kuimarika ambapo kwa sasa uchumi wa Zimbabwe unakua kwa wastani wa asilimia 3.5, mwaka ujao unatarajiwa kukua kwa wastani wa asilimia 4.2 na mwaka unaofuata kuongeza hadi wastani wa asilimi 4.4.
Kufuatia hali hiyo ameisihi Jumuiya ya Kimataifa kuondoa vikwazo mbalimbali vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe kwa kuwa vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Zimbabwe wakiwemo watoto na wanawake.
RAIS MAGUFULI NA RAIS WA ZIMBABWE WAKICHEZA WIMBO WA ‘SHAURI YAKO’