Leo April 9, 2019 Rais Magufuli amesema Wahujumu uchumi wamewahi kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutengeneza stampu hewa za Bilioni 10.
Amesema stampu hizo baada ya kutengenezwa zilisambazwa katika viwanda nchini kupitia ushirikiano wa baadhi ya wafanyakazi wa TRA.
“Kwenye suala hili la kodi hasa kwenye vinywaji kama vile bia, konyagi na spirit (vinywaji vikali) nyingine hili kidogo ni very complex (linachanganya) ndio maana Mwenyekiti hakuzungumza tulikuwa tunakusanya kiasi gani, angezungumza hilo tungekuwa tunagonga stampu tungekuwa tunakusanya ngapi, tungepata jibu vizuri” JPM
“Hatukusanyi kitu katika eneo ambalo tumepigwa sana ni hilo la vinywaji, kwa hiyo Serikali inakosa pesa hakuna mahali tulipata pesa, lazima sasa tutafute utaratibu mzuri ili hawa wenye viwanda vya vinywaji tusipoteze pesa zaidi” JPM