Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Ltd. Mfanyabiashara Rostam Aziz, amemshukuru Rais Magufuli kwa kuweka usawa wa kibiashara katika miaka minne ya uongozi wake
Rostam amesema hayo Kigamboni jijini DSM wakati wa uzinduzi wa ghala na mitambo ya gesi ya Taifa (Taifa Gas) ambayo ni gesi ya majumbani iliyozinduliwa rasmi na Rais Magufuli.
“Uimarishwaji wa sekta binafsi utatekelezwa kwa uwanja ulio sawa kama kujenga miundombinu itakayowasaida Watanzania kujikwamua kutoka katika umaskini wa kihistoria na Rais historia itakukumbuka katika hili,” Rostam Aziz
“Kuna watu walisema kuwa wewe si rafiki wa sekta binafsi nataka niwaambie kuwa uongozi wako ndiyo umefanya nianze kurudisha mitaji ya uwekezaji ambayo niliwekeza nje na Taifa Gas ni mwanzo tu ila kuna miradi mingine itakayogharimu Bilioni 500 katika miaka mitatu ijayo,” Rostam Aziz
LIVE: RAIS MAGUFULI NA ROSTAM AZIZ KATIKA UZINDUZI WA GHALA LA GESI LA TAIFA