Top Stories

DC afunguka kuamuru Mkurugenzi wake awekwe Sero Saa 24, Milioni 40 zatajwa (+video)

on

Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Aron Mbogho amefunguka juu ya taarifa iliyoenea jana January 8, 2019 kuwa ametoa amri ya kuwekwa ndani kwa Mkurugenzi wake Zefrin Lubuva nakusema hajamuweka ndani kama ilivyoripotiwa bali alipelekwa Polisi kuhojiwa kutokana nakushindwa kutoa taarifa kuhusu matumizi ya Milioni 40.

DC Mbogho anatuambia “Si kweli kwanza Mkurugenzi hakuwekwa Saa 24, ukweli ni kwamba Mkurugenzi na mwenzie walifikishwa Kituo cha Polisi kwa tuhuma ambazo zililetwa na Mamlaka ya Mji Mdogo kwamba kuna matumizi ya pesa yameleta sintofahamu” 

BREAKING: AJALI YA TRENI NA SCANIA IMETOKEA DODOMA, INADAIWA KUNA VIFO

 

Soma na hizi

Tupia Comments